Akizungumza na East Africa Radio, Ofisa Habari wa timu hiyo, Oscar Assenga amesema mchezo huo utakuwa ni kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa na michuano ya Ligi kuu Tanzania Bara Mzunguko wa Pili unaotarajiwa kuanza Desemba 26 mwaka huu.
Assenga amesema pamoja na maandalizi lakini mchezo huo utamsaidia kocha mpya wa kikosi hicho James Nandwa kuweza kutambua uwezo wa wachezaji waliowasajili katika usajili wa Dirisha Dogo, pamoja na mapungufu yaliyopo katika kikosi hicho ili kuweza kuyafanyia kazini na kuweza kuboresha kikosi hicho.
Assenga amesema wanaamini kikosi hicho kitakuwa bora katika michuano ya Ligi Kuu Tanzania Bara kutokana na mazoezi pamoja na mechi mbalimbali za kirafiki walizocheza pamoja na wanazotarajia kucheza..