Friday , 22nd Jan , 2016

Ligi kuu ya soka ya England inatarajiwa kuendelea tena wikendi hii kwa michezo kumi baada ya mapumziko kupisha mechi za FA.

Ligi kuu ya soka ya England inatarajiwa kuendelea tena wikendi hii kwa michezo kumi baada ya mapumziko kupisha mechi za FA.

Kesho Jumamosi jumla ya michezo nane itapigwa katika viwanja mbalimbali ambapo Norwich city watawaalika Liverpool, Crystal Palace watakuwa wenyeji wa Tottenham, na Leicester dhidi ya Stoke.

Mechi nyingine kesho ni Man United watakaokuwa nyumbani dhidi ya Southampton, Sunderland watachuana na Bournemouth, Watford watakuwa wenyeji wa Newcastle, West Brom watawaalika Aston Villa na Man City watakuwa wageni wa West Ham United.

Jumapili ligi hiyo itaendelea tena kwa michezo miwili ambapo Everton watakuwa wenyeji wa Swansea city na Arsenal watakuwa nyumbani Emirate dhidi ya Chelsea.

Wakati huo huo Manchester United wamekanusha taarifa za kwamba walikutana na kuzungumza na meneja wa Bayern Munich Pep Guardiola kuhusu uwezekano wa kocha huyo kuwa meneja wao.

Guardiola, mwenye umri wa miaka 45, anatarajia kuondoka Bayern Munich baada ya msimu huu na amesema amepokea maombi kutoka klabu kadhaa za Uingereza.

Manchester City wamo kwenye nafasi nzuri ya kumchukua, lakini Chelsea na United pia wanadaiwa kumnyemelea