Thursday , 10th Nov , 2016

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF limeongeza kitita cha fedha zinazozawadiwa washindi katika michuano yote kuanzia mwaka 2017 kuelekea 2020.

Mabingwa wa Afrika, Mamelod Sundowns

Washindi wa Kombe la Mataifa ya Bara Afrika (AFCON) watapata dola milioni 4, badala ya dola milioni 1.5 ya awali.

Mshindi wa Kombe la Vilabu Bingwa Afrika atajishindia dola milioni 2.5 badala ya dola milioni 1.5 za sasa.

Wakati huohuo fedha za mshindi wa Kombe la Mataifa ya Bara Afrika kwa upande wa wanawake zitaongezwa na kufikia 80,000 mwaka 2019 kutoka dola 50,000 mwaka huu.