Monday , 1st Jun , 2015

Klabu ya Yanga imesema, inasajili wachezaji kutokana na nafasi na kipaji alichonacho mchezaji ili kuboresha kikosi katika msimu ujao wa Ligi kuu Soka Tanzania Bara.

Akizungumza jijini Dar es salaam, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga, Jerry Muro amesema, Mchezaji Malimi Busungu ambaye amesajiliwa na klabu hiyo na kupewa jezi nambari 16 iliyokuwa ikivaliwa na kiungo Nizar Khalfan, walimuona msimu wa Ligi uliopita akifanya vizuri na kuonyesha kipaji dhahiri hivyo wamemsajili kwa miaka miwili.

Kwa upande wake Busungu amesema, ni malengo yake aliyojiwekea kucheza Klabu ya Yanga na anaamini yeye kama mwanajeshi daima mapambano yapo kila sehemu hivyo anaamini atafanya vizuri katika klabu hiyo.

Busungu amekabidhiwa jezi nambari 16 iliyokuywa ikitumiwa na mchezaji wa Klabu ya Yanga Nizar Khalfani ambaye ameachana na kikosi hicho na kumwaga wino timu ya Mwadui ya mjini Shinyanga.