Thursday , 18th Jun , 2015

Baraza la michezo nchini BMT limesema halitafanya uchaguzi wa viongozi wa mchezo wa Badminton yaani vinyoya lakini watakaa na wale waliochukua fomu na kuwachagua kwa muda.

Akizungumza na East Africa Radio, Afisa habari wa BMT, Najaha Bakari amesema, baada ya kuchagua viongozi wa muda watapanga tena tarehe ya uchaguzi wa chama hicho ambapo walewale waliochukua fomu ndio watakaoshiriki uchaguzi huo.

Uchaguzi wa Badminton ulitakiwa kufanyika Juni 10 mwaka huu lakini uliahirishwa tena baada ya wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi kushindwa kufika katika uchaguzi huo.