Wednesday , 24th Feb , 2016

Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini BFT limesema lina imani na mabondia waliochaguliwa katika kambi ya timu ya taifa kwa ajili ya kushiriki mashindano ya kufuzu Olimpiki yatakayofanyika Machi 09 mpaka 20 mwaka huu Yaoundé nchini Cameroon.

Katibu mkuu wa BFT Makore Mashaga amesema kikosi kimeshaanza mazoezi kwa ajili ya mashindano hayo na kitaingia kambini mwishoni mwa wiki hii.

Mashaga amesema licha ya vijana hao kuwa na uwezo mzuri wa kuiwakilisha nchi lakini pia nidhamu yao inaridhisha ndani na nje ya kazi.

Mashaga amesema kikosi hicho kimechanganyika mabondia wa zamani na wa sasa hivi ambao wana uwezo mkubwa wa kuweza kuipeperusha bendera ya taifa katika mashindano ya kufuzu ushiriki wa Olimpiki.

Makore amesema wamejipanga kupeleka mabondia nane makocha wawili, viongozi wawili ambapo mmoja atatoka katika shirikisho na mmoja kutoka serikalini.