Thursday , 2nd Jun , 2016

Bingwa wa zamani wa mbio ndefu duniani Haile Gebreselassie amelalamikia shirikisho la riadha nchini Ethiopia kwa kumwacha bingwahuyo wa mara tatu wa mashindano ya Olimpiki, Kenenisa Bekele nje ya kikosi cha taifa hilo.

Kikosi cha riadha nchini humo kinatarajia kuelekea katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Jeneiro mwezi Agosti.

Haile amesema kwamba Bekele alistahili kuorodheshwa katika kikosi cha Marathon bila pingamizi lolote kutokana na rekodi yake nzuri.

Shrikisho la riadha nchini Ethiopia linasema kuwa Bekele aliachwa kwa kuwa hakuafikia mahitaji ya kikosi hicho.

Hata hivyo Bekele amekosoa uamuzi huo akisema haukuwa wa haki.

Bekele alikuwa wa tatu katika mashindano ya London marathon yaliyofanyika mwezi Aprili, licha ya kutofanya mazoezi kamili na alishinda mbio za marathon za 'Great Manchester Run' mwezi uliopita.

Chanzo BBC