Monday , 3rd Nov , 2014

Mashindano ya kimataifa ya kirafiki ya Mpira wa Miguu wa Ufukweni yanatarajiwa kufanyika Desemba Mosi mpaka Saba mwaka huu visiwani Zanzibar kwa kushirikisha timu kutoka Nchini Uganda,Tanzania Bara na wenyeji Zanzibar.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa kamati ya Beach Soka Zanzibar, Ally Adolf amesema lengo hasa la michuano hiyo ni kulishawishi Shirikisho la Soka Afrika Mashariki na Kati CECAFA kuandaa mashindano kwa nchi za Afrika Mashariki na kati.

Adolf amesema kabla ya kuanza kwa mashindano hayo kutakuwa na semina ya siku moja kwa viongozi pamoja na wachezaji ili kuweza kuelewa jinsi michuano hiyo itakavyoanza.