Tuesday , 16th Jun , 2015

Watu wasiojulikana wamelishambulia kwa mawe basi la timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars maeneo ya Kariakoo, jijini Dar es Salaam.

Basi hilo lililokuwa limebeba baadhi ya wachezaji wa timu hiyo waliokuwa wakitoka mazoezini uwanja wa Karume, lilishambuliwa kwa mawe na watu wanaosadikiwa kuwa mashabiki wenye hasira.

Taifa Stars juzi ilifungwa mabao 3-0 na Misri katika mechi yake ya kwanza ya Kundi G kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika 2017 mjini Alexandria.