Thursday , 9th Jul , 2015

Mashindano ya Taifa ya mchezo wa Baseball yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Desemba 10 mpaka 14 jijini Dar es salaam kwa kushirikisha zaidi timu kutoka timu za shule za Sekondari hapa nchini.

Akizungumza na East Africa Radio, Katibu mkuu wa Chama cha Baseball na Soft Ball nchini, Alpherio Nchimbi amesema wamelenga zaidi kwa shule za Sekondari ili kuweza kuendelea kupata vipaji kutoka kwa vijana hao ambao wanaamini wataendelea kufanya vizuri zaidi.

Nchimbi amesema, wanafunzi katika shule mbalimbali mikoani wanaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na michuano hiyo.

Nchimbi amesema, watatumia mashindano hayo kuchagua vijana watakaounda timu ya Taifa ambayo itashiriki mashindano ya Afrika Mashariki yatafanyika Desemba nchini Uganda.