Friday , 22nd Aug , 2014

UONGOZI wa Klabu ya Coastal Union ya Tanga umemfungia aliyekuwa beki wa kushoto Abdi Banda kucheza mpira wa miguu ndani na nje ya nchi kwa kipindi cha mwaka mmoja baada ya kukosa nidhamu na kusaini mikataba katika vilabu viwili tofauti.

Adhabu hiyo itahusisha kutokucheza mechi zozote ikiwemo zile za kirafiki kutokana na kukiuka makubaliano aliyoingia na klabu hiyo ya Coastal Union wakati aliposajiliwa.

Akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari leo,Katibu wa Coastal Union,Kassim El Siagi alisema kuwa uongozi umeamua kumpa adhabu hiyo kwa kukosa nidhamu pale aliposaini mkataba mwengine na timu ya Simba SC ya Dar es Salaam wakati akijua tayari ana mkataba wa miaka mitatu na timu ya Coastal Union.

El Siagi alisema kuwa mchezaji huyo alikuwa amebakiza miaka miwili kucheza timu ya Coastal Union na hivi sasa yupo katika mikataba miwili kwa timu mbili tofauti ambazo zinashiriki ligi moja.

“Ki ukweli hali hii hatuweza kuivumilia ndio maana tumeamua kuchukua hatua hiyo kali ili iweze kuwa fundisho kwa wachezaji wengine wenye tabia kama hii “Alisema Katibu El Siagi.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo mchezaji huyo atakuwa amevunja sheria na kanuni za mchezo wa mpira wa miguu hapa nchini na kulitaka shirikisho la soka kutoa ushirikiano katika maamuzi hayo.