Rais wa Chama cha Waendesha Baiskeli Tanzania, Godfrey Jacks Muhagama,akiwa miongoni mwa waendesha baiskeli kwenye mashindano jijini Mbeya.
Akizungumza na East Africa Radio Rais wa chama hicho Godfrey Mhagama amesema wanatarajia kufanya kikao mapema mwakani ili kuanza maandalizi ya ushiriki wao kwenye mashindano husika.
Mhagama amekiri kuwa kwa muda wa takribani miaka saba wameshindwa kuandaa mashindano ya kitaifa kutokana na kukosa udhamini wa uhakika lakini tayari wamekwisha kuanza mazungumzo na baadhi ya makampuni ili kuweza kuwaunga mkono kwenye hilo.
Ameongeza kuwa tayari yeye kama kiongozi pamoja na wenzake wanatatua matatizo yanayokisibu chama chao ili kiweze kuwaandaa wachezaji ambao wataisaidia Tanzania kuleta medali kwenye mashindano ya kimataifa.