Thursday , 7th Jan , 2016

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa amesema bado anamfuatilia mshambuliaji wa Tanzania Yusufu Adi anayecheza kwenye klabu ya Mansfield Town ya ligi daraja la pili nchini Uingereza.

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Charles Boniface Mkwasa amesema bado anamfuatilia mshambuliaji wa Tanzania Yusufu Adi anayecheza kwenye klabu ya Mansfield Town ya ligi daraja la pili nchini Uingereza.

Mkwasa ambaye kikosi chake kinajiandaa na mchezo wa kufuzu AFCON 2017 dhdi ya Chad mwezi Machi mwaka huu, amesema awali alishindwa kumwita Adi kwasababu alikuwa bado yupo kwenye madaraja ya chini, lakini tangu atue Mansfield amekuwa akipata nafasi ya kuonekana.

Adi mwenye umri wa miaka 23,aliitwa kwenye kikosi cha Stars kwa mara ya kwanza Agosti mwaka uliopita kwenye kambi ya Stars nchini Uturuki kujiandaa na Nigeria,lakini aliachwa kutokana na majeruhi.

Adi mzaliwa wa visiwani, Zanzibar,alijiunga na Mansfield Town Juni 5 mwaka 2015, akitokea klabu ya Oxford City inayocheza ligi ya Conference North, kabla ya hapo alishawahi pia kuchezea Academy ya klabu ya Leicester City inayocheza ligi kuu ya soka nchini Uingereza, kuanzia 2008-2011.

Kwa sasa Stars haina mchezaji anayeeleweka katika kusakata kabumbu Ulaya hasa kwenye ligi kubwa na wengi waliopo huko ni wale wanaokwenda kucheza kwa kujifurahisha na kuishia na maisha mengine.

Habari nzuri kwa sasa ni mpango wa Mbwana Samatta, kutakiwa na klabu ya KRC Genk iliyopo ligi kuu ya soka nchini Ubelgiji, huku mwenza wake kwenye klabu ya TP Mazembe Thomas Ulimwengu akitakiwa Ufaransa.