Monday , 28th Apr , 2014

Bodi ya ligi ya soka nchini Tanzania (TPLB) imesema kuwa imeridhishwa na ushindani uliojitokeza katika ligi kuu Tanzania Bara (VPL) na ligi daraja la kwanza (FDL) ambazo zimemalizika hivi karibuni.

moja kati ya michezo ya ligi kuu Tanzania bara

Bodi ya ligi ya soka nchini Tanzania (TPLB) imesema kuwa imeridhishwa na ushindani uliojitokeza katika ligi kuu Tanzania Bara (VPL) na ligi daraja la kwanza (FDL) ambazo zimemalizika hivi karibuni.

Ofisa wa bodi hiyo Joel Balisidya amesema kuwa ushindani katika ligi hizo pamoja na nidhamu iliyooneshwa na wachezaji kwa kiasi kikubwa ndiyo vimechangia kuwepo na ubora wa ligi hiyo msimu huu.

Aidha Balisidya amesema kuwa matokeo ya mwisho ya ligi hiyo nayo yametoa picha halisi ya jinsi ushindani ulivyokuwa mkubwa mpaka dakika ya mwisho, ndipo timu zilizopanda daraja kwa upande wa ligi daraja la kwanza zikajulikana na pia bingwa wa ligi kuu kupatikana.