Mashabiki wa Yanga
Yanga imetolewa katika mchezo wa kwanza ambapo michuano hiyo huanzia hatua ya robo fainali. ''Kwasasa imekuwa rahisi tu Yanga kufungwa baada ya Jacob Massawe kuwafunga'', amesema Manara.
Yanga sasa imeungana na Singida United kuwa timu mbili ambazo zimeaga mashindano ya SportPesa baada ya Singida United kufungwa bao 1-0 na Bandari FC kwenye mchezo wa mapema leo.
Mabao ya Kariobangi Sharks yamefungwa na Abuya Duke aliyefunga mawili pamoja na Abege George aliyefunga moja. Huku yale ya Yanga yakifungwa na Amissi Tambwe na Heritier Makambo.
Kesho Simba itashuka dimbani kucheza na AFC Leopard huku mabingwa watetezi Gor Mahia wakicheza na Mbao FC ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza.







