
Kikosi cha Azam FC
Hatua hiyo imekuja ikiwa ni nia ya Azam FC kutaka kufanya vizuri zaidi kwenye mzunguko wa pili wa ligi, Kombe la Shirikisho na Michuano ya Kimataifa inayokuja kuanzia mwezi ujao na mwakani (Kombe la Kagame na lile la Shirikisho Afrika).
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Yeray Romero, alisema kuelekea mzunguko wa pili wa ligi wanatarajia kuangalia mapungufu ya kikosi hicho kabla ya kuingiza sura mpya kwenye usajili ya dirisha dogo kwa ajili ya kuinyanyua timu na kufika kwenye nafasi nzuri zaidi.
“Wakati wachezaji wapya wanaingia pia tunatarajia kuwaangalia wachezaji ambao tunadhani kwa sasa kikosini hawawezi kuisaidia timu, ambao ndiyo watawapisha wachezaji hao, lengo la yote haya ni kuweza kuipeleka mbele zaidi timu zaidi ya hapa ilipo,” amesema Romero.
Romero pia amewapongeza wachezaji kwa kazi waliyoweza kuifanya mpaka sasa huku wao kama benchi la ufundi wakiahidi kufanya kazi nzuri zaidi kwa asilimia 100 katika kuirekebisha zaidi timu na kuziba mapungufu yaliyopo.
Azam FC imemaliza mzunguko wa kwanza ikiwa na pointi 25 ambapo imefanikiwa kucheza jumla ya mechi 15 kwenye mzunguko wa kwanza wa ligi ikifanikiwa kushinda jumla ya mechi saba, sare nne na kupoteza michezo minne.