Sunday , 2nd Aug , 2015

Azam FC wanakuwa timu ya kwanza ya Tanzania nje ya Simba na Yanga SC kutwaa taji hilo- wakishiriki kwa mara ya tatu tu mashindano hayo baada ya mwaka 2012 walipofika fainali na kufungwa na Yanga SC 2-0 Dar es Salaam na mwaka jana kutolewa kwa penalti

Kikosi cha mabingwa wapya wa kombe la Kagame 2015/2016 timu ya Azam FC ya Tanzania.

Azam fc ya Tanzania imetawazwa mabingwa wapya wa soka wa michuano ya klabu bingwa kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati [maarufu kombe Kagame] mara baada ya kufanikiwa kuwachapa Gor Mahia ya Kenya mabao 2-0 katika mchezo mkali ambao Gor Mahia iliyowahi kutwaa ubingwa huo mara tano ilikuwa ikiwania ubingwa huo kwa mara ya sita Tangu ilipofanya hivyo mnamo mwaka 1985 ikiwa ni miaka 30 iliyopita huku Azam FC ya Tanzania inayonolewa na kocha Muingereza Stewart John Hall aliyewahi kuifikisha fainali za Kagame mwaka 2012 ikiweka rekodi yakutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza.

Mchezo huo wa fainali Ulitanguliwa na mchezo wakutafuta mshindi wa tatu baina ya Al Khartoum na KCCA na KCCA kufanikiwa kutwaa nafasi hiyo baaada ya kuibuka na ushindi wa bao 2-1 nakutwaa medali za shaba.

Magoli Mawili ya Azam fc ambayo ilionyesha kandanda safi hii leo nakuipteza kabisa Gor Mahia iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa kutwaa kombe hilo yalifungwa na mshambuliaji Ngongoti John Bocco [adebayor[ na la pili likifungwa kiufundi kwa mkwaju wa faulo na mshambuliaji Kipre Tchetche na kufuta kabisa ndoto za Gor Mahia iliyokuwa ikiwania kufikia rekodi ya Simba ambayo imetwaa kombe hilo mara sita rekodi ambayo pia iliwaniwa na Yanga ambayo ilitolewa katika hatua ya robo fainali.

Kwaushindi huo Azam fc ambao ndio mabingwa wapya wa kombe la Kagame wanatwaa medali za dhahabu na kitita cha pesa taslim dola za Marekani elfu 30 huku Gor Mahia wakitwaa dola elfu 20 na medali za fedha na washindi wa tatu KCCA wakitwaa medali za shaba na kiasi cha dola 10.

Timu hiyo yenye maskani yake Azam Complex, Chamazi, Mbade, Temeke mjini Dar es Salaam imeweka rekodi ya kushinda mechi zake zote kuanzia Kundi C bila kuruhusu nyavu zake kuguswa hata mara moja- na ‘ilipata shida’ kidogo tu mbele ya Yanga SC katika Robo Fainali ilipolazimika kushinda kwa penalti 5-3 baada ya sare ya 0-0 dakika 90, wakati Nusu Fainali iliilaza KCCA 1-0.