
Donald Ngoma
Akizungumza katika mahojiano maalum na kipindi cha Kipenga cha East Africa Radio, Ngoma ametupa lawama kwa baadhi ya watu anaodai kuwa wana lengo la kumgombanisha nauongozi wa klabu hiyo kwa kumzushia maneno.
Ngoma ambaye amekuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu kutokana na majeraha, amesema hana mgogoro wowote na uongozi wake, huku akikanusha tetesi za kutumiwa na timu nyingine zinazoshiriki ligi kuu Tanzania Bara, kuihujumu timu yake.
Amesema kubwa linalomsibu ni majeraha na kuwataka mashabiki wa Yanga wamuelewe na kupuuza maneno yanayosambaa kuwa amegoma kucheza.
Kuhusu mkataba, amesema mkataba wake unamalizika mwezi Juni mwaka huu, na bado hajaamua hatma yake kama ataendelea kubaki Yanga au ataondoka.
katibu wa Yanga Boniface Mkwasa amesema kuwa mchezaji huyo bado ni majeruhi na hataweza kuungana na kikosi cha Yanga kinachoelekea Morogoro.
Msikilize hapa alipokuwa akifanya mahojiano na Crispin Hauli 'Kiberenge' wa kipindi cha Kipenga