Sunday , 26th Jun , 2016

Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel Tanzania imezindua mashindano ya vijana, chini ya umri wa miaka 17, Airtel Rising Stars kwa msimu wa 6 hii leo, makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dare se Salaam.

Kampuni ya simu za mkoni ya Airtel Tanzania imezindua mashindano ya vijana, chini ya umri wa miaka 17, Airtel Rising Stars kwa msimu wa 6 hii leo, makao makuu ya kampuni hiyo jijini Dare se Salaam.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo, Mkurugenzi wa Mahusiano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano, amesema bado kampuni yao itaendelea kudhamini mashinado hayo kwa lengo la kuwapa fursa vijana kupata ajira na kujitegemea kiuchumi.

Amesema mashindano ya mwaka huu, yatatoa fursa kwa vijana katika mikoa ya Mwanza, Morogoro, Lindi, Arusha, Mbeya, Zanzibar, pamoja na Mikoa ya kisoka, ya Kinondoni, Ilala na Temeke, na hivi karibuni, taarifa ya maeneo ya kujisajili kwa vijana hao, itatangazwa.

Naye Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Nape Nnauye, ambaye alikuwa mgeni rasmi, wa tukio hilo, amewaagiza viongozi wa mpira wa miguu mikoani, kuyapa kipaumbele mashindano ya Airtel Rising Stars, yanayotoa ajira kwa vijana.