Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

VIDEO: Chadema hawana Shukrani - Wolper

Thursday , 25th May , 2017

Malkia wa filamu bongo, Jacqueline Wolper amefunguka sababu za kuacha kuendelea kuisapoti CHADEMA ni viongozi wa chama hicho kushindwa kuutambua mchango wake alioutoa wakati wa uchaguzi mkuu hali iliyomfanya ajihihisi mpweke na kama ametelekezwa .

 Wolper na baadhi ya Wasanii wakati wa kampeni za Uchaguzi mkuu 2015.

Ikiwa ni mara ya kwanza Wolper kufunguka ishu hiyo katika kipindi cha KIKAANGONI kinachorushwa kwenye ukurasa wa facebook EATV, amesema hajawai kuwa msaliti kwani hakuwa mwanachama wa chama hicho lakini alisikitishwa na uongozi wa chama kushindwa hata kumshukuru kwa kazi aliyoifanya wakati wa uchaguzi mkuu kwa kujitoa pasipo kulipwa hata shilingi elfu 10 za kitanzania.

Pamoja na kuwa alifanya kampeni za kumsapoti Mgombea uraisi kupitia mwamvuli wa UKAWA Mhe. Edward Lowassa, Wolper amedai kuwa hakuwa anasapoti chama kizima bali mgombea kwa kuwa yeye ni shabiki wa kiongozi huyo na familia yake kwa ujumla ndiyo maana hakukubali kulipwa katika kampeni hizo.

Wolper akiwa Kikaangoni

 "Mimi nilifanya siasa kwa sababu namkubali Lowassa, na mimi ni shabiki wake na familia yake kwa ujumla. Nilianza kumsapoti Lowassa tangu yupo CCM. Mimi ni mfanyabiashara na muigizaji, sijawahi kuwa mwanasiasa ndio maana nilikuwa namsapoti mtu mmoja mmoja na siyo chama. Hata hivyo mimi siyo Yuda kwa CHADEMA kwa sababu sijawahi kuwa mwanachama wao na sina chama  chochote lakini wao baada ya uchaguzi walinitelekeza kiasi cha kunifanya nijisikie mpweke. Hata kama hawakushinda uchaguzi walipaswa hata viongozi wawili wanishukuru tu kwa maneno ili na mimi nipate faraja lakini hawakuweza kufanya hivyo.

Hata hivyo Wolper amekiri wazi hata tatizo na Mhe Lowassa na hawezi kuml;aumu kwa yaliyotokea bali atakuwa naye bega kqwa bega tena kumsapoti endapo atapata tena nafasi ya kugombea urais 2020.

Mtazame hapa chini Wolper akifunguka kwa undani zaidi.

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali