
Staa wa muziki nchini Uganda Ziggy Dee
Ziggy Dee ambaye mpaka sasa ameweza kukamilisha albam moja ya muziki wa injili, ameeleza kuwa anafurahia upande aliopo sasa, akijitapa pia kuwa anawakubali zaidi mashabiki wa muziki wa Injili kuliko wale wa muziki wa kidunia aliokuwa anaufanya.
Star huyo ambaye alijizolea umaarufu mkubwa kupitia rekodi ya Eno Mic, licha ya yote hayo, amekiri kuendelea kutumia kilevi kidogo, ikiwepo kuvuta jani, akijitetea kuwa hakuna jipya katika maisha ya kidunia, akiwa amepunguza sana anasa na starehe za kidunia.
