Yamoto Band
Kundi la muziki la Yamoto Band, wakiwa sasa wanatamba na ngoma yao mpya ya Cheza Kwa Madoido ambayo kama ulikuwa hufahamu ni project ya kwanza kabisa kufanya na producer tofauti na Shirko ambaye ndiye amekuwa akiwasukia hitz zao zote, wamezunguzia utofauti wa kubadili jiko la kupikia kazi ambapo wamesema wanajivunia wepesi wa kubadilika badilika na uwezo wa kufanya kazi na producer yoyote.
Kupitia mahojiano ambayo tumefanya na wakali hawa, kufanya kazi yao mpya na mtayarishaji muziki Mesen Selekta imekuwa ni mafasi nyingine kuonyesha uwezo na pia kutoa burudani kwa mashabiki wao ambao ni kutoka kila rika ndani ya jamii/
Vilevile wasanii hawa hawakuacha kutambua mchango wa mkubwa Fella katika kusuka rekodi nzima ya Cheza Kwa Madoido kuanzia wazo lake na kugusia pia kuwa, video ya kazi hiyo itakuwa ni kubwa zaidi kuliko zile ambazo wamewahi kufanya, ikiwa ni ahadi ya nguvu kutoka kwa meneja wao, Mkubwa Fella.