Monday , 22nd Jun , 2015

Kundi la Muziki la Ya Moto Band wako mbioni kufanya Colabop na msanii mkubwa kutoka nchini Nigeria ambapo kwa sasa muziki kutoka huko ndio umeiteka Afrika.

Yamoto Band

Meneja wa Kundi Hilo Said Fella amesema bado hawajajua ni msanii gani atakaye fanya kolabo na Ya Moto Band ila mipango inaendelea nchini Afrika Kusini chini ya Mtayarishaji wa Video kali GodFather.

Aidha Mkubwa Fella amesema amerejea Tanzania ili kuweka mambo sawa ambayo walishindwa kuelewana na Mamlaka ya Mapato nchini Tanzania Jinsi ya kuuza Album ya kundi hilo