Thursday , 15th Oct , 2015

Msanii wa muziki wa kimataifa kutoka Nigeria, Wizkid anaendelea kutisha na rekodi mbalimbali ikiwepo kutajwa kuwania tuzo maarufu za Headies za huko Nigeria katika vipengele zaidi ya sita.

Msanii wa muziki wa kimataifa kutoka Nigeria Wizkid

Katika vipengele hivyo sita nyota huyo alivyotajwa kuwania ni Rekodi ya Mwaka, Albam bora ya RnB na Pop, Wimbo Bora wa Pop, Kolabo Bora, Albam ya Mwaka, Msanii bora wa Mwaka na wimbo Bora wa Mwaka.

Wizkid ambaye alianza muziki akiwa na umri wa miaka 11 akijulikana kama Lil Prinz, katika tuzo hizo anapambana na wasanii wengine wakali, akitokea katika vichwa vya habari kutokana na jina lake kutokea katika vipengele vingi zaidi, sambamba na msanii wa muziki Olamide.

Nyota huyo anatarajiwa kutua Dar es Salaam, kwaajili ya onesho kubwa kabisa la Wizkid Live in Dar tarehe 31 mwezi huu, ndani ya viwanja vya Leaders Club, tukio kubwa kabisa la burudani la kihistoria ambalo huna sababu ya kulikosa.