Wednesday , 2nd Sep , 2015

Rapa Witnesz ameonyesha kuguswa na kubezwa na watu kwa njia ya mtandao, kufuatia kuweka picha akiwa na viongozi wa juu wa nchi, akifafanua kuwa picha hizo hazimaanishi kwa vyovyote mpaka sasa kama kuna upande ana usapoti kisiasa.

Witnesz na Dulla wa Planet Bongo East Africa Radio/TV

Katika kipindi hiki ambacho kumekuwa na makundi ya wasanii waliogawanyika na kuonesha waziwazi misimamo yao kisiasa, Witnesz anakuwa ni kati ya wale ambao wanaona bado kuna umuhimu wa kutulia na kufuatilia mchakato mzima kabla ya kufanya maamuzi kama anavyoeleza hapa.

Tags: