Saturday , 9th Aug , 2014

Mwigizaji maarufu wa filamu hapa Bongo, Wastara Juma ameweka wazi kuwa baada ya kukamilika kwa filamu yake mpya ya Last Decision, amejipanga kwaajili ya uzinduzi wa aina yake ambao ataufanya mitaani pamoja na mashabiki wake ndani ya siku 5 zijazo.

Wastara Juma

Wastara amesema kuwa, atatumia siku nzima katika kuzindua kazi hii katika wilaya za jiji la Dar pamoja na kukutana na mashabiki wake ambao kwa asilimia kubwa wanapatikana huko mitaani.

Wastara pia katika mahojiano tuliyofanya naye, amekanusha taarifa za yeye kupata mchumba na kuolewa huko Uingereza, na kufafanua kuwa picha zilizokuwa zimesambaa mitaani juu ya hili, ni kutoka katika scene ya filamu.