Kadjanito ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa kutumia njia za mkato si mzuri, na zitawafikisha pabaya.
“Wasichana tumekuwa na tamaa sana tunataka sana shortcut, shotcut sio nzuri utafika lakini haitadumu kwa muda mrefu, kwa hiyo tujifunze kutengeneza njia ndefu ambayo hata kama itachukua muda lakini matunda yake yakija kutoka utafurahia siku zote”, alisema Kadjanito.
Pamoja na hayo msanii huyo amewataka wasichana kuwa na moyo wa uthubutu na kutokuwa na tamaa, na kujiamini katika kile wananchotaka kufanya.
“Kikubwa kufocus na kutokuwa na tamaa, tujitambue, tusijione kama sisi wanawake hatuwezi, tujipe kipaumbele tujaribu kila kitu ambacho tunaweza kuamini kinaweza kutufanya tukawa watu fulani, tusiogope”, alisema Kadjanito.