Monday , 31st Aug , 2015

Baada ya kumalizika kwa hatua ya Robo Fainali ya mashindano makubwa ya Dance 100% 2015 mwishoni mwa wiki, Mratibu wa mashindano hayo kutoka upande wa BASATA, Kwerugira Maregesi ametoa wito kwa makundi yaliyoingia nusu fainali.

Mratibu wa mashindano hayo kutoka BASATA, Kwerugira Maregesi

Maregesi ametaka madansa wanaounda makundi hayo kuongeza mazoezi na juhudi kutokana na ukubwa wa mashindano hayo Afrika Mashariki, kufahamu kuwa hii ndio nafasi ya wao kuonekana na kupata mashavu ya kibiashara, ubunifu na mitindo mipya ikiwa ndiyo siri pekee ya kufanikiwa kusonga mbele.

Maregesi pia ameeleza kufurahishwa na kuzidi kupiga hatua kwa mashindano hayo akiwataka madansa pia kulizoea jukwaa jipya na bora ambalo limeanza kutumika kama sehemu ya maboresho ya mashindano.