Tuesday , 8th Nov , 2016

Zikiwa zimebaki siku 33 kutolewa kwa Tuzo za EATV ambazo zinahusisha wasanii wa muziki pamoja na wasanii wa filamu nchini, East Africa Television leo imetangaza wasanii ambao wamefanikiwa kuingia katika baadhi ya vipengele vya tuzo hizo.

Dominician Mkama - Mkuu wa Kanda Dar es Salaam kutoka Vodacom Tanzania, akitaja majina ya wasanii wanaowania tuzo hizo, ndani ya studio za EA Radio

Akizungumza kupitia kipindi cha Planet Bongo ya East Africa Radio Dominican Mkama, Mkuu wa Mauzo Kanda ya Dar es Salaam kutoka Vodacom amewataja wasanii watano wanaowania kipengele cha 'Muigizaji Bora wa Kiume' na wanamuziki watano wanaowania kipengele cha "Mwanamuziki Bora Chipukizi"

MUIGIZAJI BORA  WA KIUME 

Nominee: Saidi Ally filamu aliyoigiza (Ndugu wa mume)

Nominee: Meya Shabani Hamisi filamu aliyoigiza (Facebook profile)

Nominee: Salim Ahmed (Gabo) filamu aliyoigiza (Safari ya Gwalu)

Nominee: Dotto Husein Matotola filamu aliyoigiza (Likwacha lala) 

Nominee: Daudi Michael Tairo filamu aliyoigiza (Mfadhili wangu)

MWANAMUZIKI BORA CHIPUKIZI 

Nominee: Amani Hamisi (Man Fongo); Wimbo - Haina Ushemeji

Nominee: Feza Kessy; Wimbo - Sanuka 

Nominee: Rukia Jumbe (Rucky baby) ; Wimbo - Give Me Some More

Nominee: Mayunga Nalimi (Mayunga) ; Wimbo - Nice Couple

Nominee: Rashid Said (Bright) ; Wimbo - Nitunze 

Zoezi la kutaja wasanii waliofanikiwa kushiriki katika tuzo za EATV (EATV AWARDS) litakuwa ni la siku nne kuanzia leo Jumanne hadi siku ya Ijumaa baada ya hapo zoezi litarudi kwa mashabiki na wananchi kwa ajili ya kuanza kupiga kura kwa wasanii ambao wanashiriki katika tuzo.

Tuzo hizo zinatarajiwa kutolewa Desemba 10 mwaka huu jijini Dar es Salaam.

Tags: