Monday , 29th Jun , 2015

Serikali kupitia Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia ameeleza kuwa kuna umuhimu wa wasanii wa muziki wa kizazi kipya, kujinoa zaidi kielimu kuboresha sanaa zao, kwa Taasisi ya Sanaa ya Bagamoyo TASUBA.

Naibu Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo Mhe. Juma Nkamia

Mhe. Nkamia amesema hayo akijibu swali la mbunge wa viti maalum, Mariam Msabaha kuhusiana na mkakati wa Serikali kuhakikisha wasanii wote wa muziki wa kizazi kipya wanajiendeleza kielimu, akihimiza pia wasanii hawa kuona umuhimu wa kusoma na kukitumia vizuri chuo hicho.