
Christina Shusho
Akiongea kupitia eNewz ya EATV, Shusho amesema wasanii wa nyimbo za injili wanapenda kuishi maisha yao halisi siku zote na hawapendi kuingiza maisha ambayo siyo yao ili kuwadanganya mashabiki zao wanaowafuatilia kwamba wanaishi maisha mazuri wakati siyo kweli.
Pia Shusho amesema watu maarufu wanapaswa kutambua kwamba kuna watu ambao wanafuatilia kila kitu wanachokifanya katika maisha yao hivyo wanawaharibia maisha wanapowadanganya mashabiki wanaowafatilia