Friday , 4th Dec , 2015

Rapa Wakazi kutoka hapa Tanzania amepata nafasi kubwa ya kuwania Tuzo za Kimataifa za Kora kwa mwaka 2016 katika kipengele cha Best Hip Hop kupitia rekodi yake ya Dengue Fever akichuana na marapa wakubwa kabisa kutoka nchi mbali mbali Afrika.

Tuzo maarufu za muziki za KORA

Katika orodha hiyo pia, msanii Mrisho Mpoto anatokea katika kipengele cha Best Tradition Male Artist of Africa, YAMOTO BAND wanatokea katika kipengele cha Most Promising artists , akiwepo pia Vanessa Mdee katika kipengele cha Best Female East Africa na Best Collabo kati ya wasanii wengine.

Kwa niaba ya wasanii hawa kuhusiana na nafasi hii, huyu hapa Wakazi na Mrisho Mpoto na pia Said fella wanaeleza furaha yao.