
Wanatetemeka Video Set
Kazi hii ikiwa kama moja ya projekti kubwa kabisa kwa Queen Darleen kuwahi kufanya, ndani yake akiwa ameshine vilivyo na Msanii Diamond Platinumz ambaye ni kaka yake wa damu, eNewz imepata nafasi ya kumegewa kipande kifupi tu cha kazi hii kutoka kwa muongoza video yenyewe Jerry Mushala ambacho utapata kukitazama katika show leo saa mbili kasoro usiki EATV pekee.