Tuesday , 28th Oct , 2014

Rapa Wakazi ambaye kwa sasa ndiye msimamizi halali ama meneja wa msanii Lady Jay Dee, amesema kuwa mbali na undugu wake na msanii huyu, tayari ameanza harakati za kumfanya Jide kuwa juu zaidi.

Lady Jay Dee, Dabo na Wakazi

Wakazi ambaye amechukua mikoba ya Garder G Habash katika kufanya kazi hii, amesema kuwa kwa sasa msanii wake anapumzika na pia kufanya kazi huku akimtengeneza zaidi katika maswala kama ya mtandao kama ambavyo inakuwa kwa wasanii wengine wakubwa.