
Hashim Kambi
Hashim amesema kuwa, binafsi alishawishiwa kuanza kuigiza baada ya nafasi za uhusika wa watu wazima katika filamu kuwa zinafanywa na watoto, hivi sasa kukiwa na watu wazima wasiozidi watano katika tasnia hiyo nzima.
Hashim Kambi amesema kuwa kwa sasa hali imekuwa tofauti baada ya watu kuanza kuona umuhimu na nafasi ya sanaa katika jamii, ambapo watu wa rika tofauti wameendelea kufunguka na kushiriki katika tasnia hiyo.