Thursday , 2nd Oct , 2014

Msanii Vitali Maembe amesema kuwa, kutokana na muelekeo wa nchi ya Tanzania kwa sasa, ameamua kuwekeza nguvu zake kutumia sanaa yake kupigia kelele haki ya watanzania hasa katika swala la umiliki wa Ardhi ambao ni nguzo ya maendeleo ya wananchi.

Akilinganisha na nguzo za maendeleo ya nchi, Watu, ardhi Siasa Safi na Uongozi bora, Vitali amesema katika hali halisi sasa, asilimia kubwa ya watu hukosa haki ya msingi ya umiliki wa ardhi wakati kuna wachache wenye ardhi kubwa.

Hivi sasa msanii huyo anaendeleza harakati zake kimuziki kuwahamasisha watanzania kujitambua katika sekta mbalimbali za kimaendeleo kutokana na vipaji na sanaa zao nchini.