Tuesday , 30th Aug , 2016

East Africa Television Limited imetoa vigezo anavyotakiwa kuwa navyo msanii wa muziki au filamu, ili kuweza kushiriki kwenye tuzo kubwa kwa Afrika Mashariki, EATV AWARDS.

Tuzo hizo ambazo kwa mara ya kwanza ndizo zinafanyika mwaka huu, zinahusisha wasanii wote wa muziki na filamu, na waliosajiliwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

Kwa mujibu wa Idara ya Masoko ya EATV, vigezo ambavyo msanii anatakiwa awe navyo ni kama ifuatavyo.

1. Awe amejiandikisha katika Baraza la Sanaa katika nchi yake ndani ya Afrika Mashariki.

2. Kazi za msanii atakazoruhusiwa kupendekeza ni zile zilizotolewa kuanzia tarehe 01/07/2015 mpaka tarehe 30/06/2016.

3. Msanii au meneja wake atatakiwa kupendekeza kazi yake kwenye vipengele vilivyotajwa.

4. Msanii anatakiwa kujaza fomu za kujipendekeza ambazo zitapatikana kwenye tovuti ya www.eatv.tv/awards au katika ofisi za East Africa Television zilizopo Mikocheni, Dar es salaam Tanzania, na kwamba zoezi la kujipendekeza ambalo ni kuchukua fomu na kurudisha fomu litakuwa ni la mwezi mmoja pekee.

EATV AWARDS ndiyo tuzo kubwa za kwanza kushirikisha wasanii wa nchi tatu za Afrika Mashariki moja kwa moja, na zinatarajiwa kufanyika mwezi Desemba mwaka 2016.

Kwa taarifa zaidi endelea kufuatilia tovuti hii pamoja na mitandao kijamii ambazo ni Facebook.com/eatv.tv, Twitter ya @earadiofam na @eastafricatv huku ukisikiliza East Africa Radio na kutazama East Africa Television