Thursday , 11th May , 2017

Msanii wa bongo fleva na mkali wa R&B, Rama Dee amchana Waziri Mkuu mstaafu wa awamu ya nne Mhe. Edward Lowassa kwa kumwambia apumzike kujihusisha na siasa ili vijana wapige kazi.

Rama Dee amebainisha hayo katika kipindi cha KIKAANGONI ambacho kinarushwa kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV kila siku ya Jumatano kuanzia saa nane mpaka saa kumi jioni.

Lowasa anapaswa apumzike awaachie watu wafanyekazi…Kwa kawaida umri wa wazee wetu wakifika umri wa miaka 55 au 60  ni umri wa kupumzika kwa kuwa wamekuwa tayari wamezeeka”. Alisema Rama dee

Aidha, Rama dee aliendelea kusema kuwa Mhe. Lowassa kwa sasa anapaswa atafute mtu wa kumrithi nafasi yake nasiyo kuendelea tena katika harakati za masuala ya kisiasa na mengineyo.

“Nafikiri yeye angeweza ku-focused kwa kumtafuta mtu ambaye ataweza kuishika ile nafasi yake naimani itakuwa vizuri zaidi”. Aliendelea kusema Rama dee