Saturday , 13th May , 2017

Wakazi amedai kwamba sababu za kutokuwepo kwa ma MC's wakali Nikki Mbishi pamoja na One The Incredible kwenye kundi lao la muziki linalokwenda kwa jina la SSK 'Sisi sio kundi' zinatokana na  kuwa na mawazo tofauti kwenye biashara ya muziki.

Wakazi amefunguka hayo kutokana na watu kuhoji kutokuwepo kwa wasanii hao ambao ni watu wakaribu zaidi kwao na kufafanua kwamba hawakuwahi kumfikiria Nikki Mbishi kuwa sehemu ya kundi lao kwa sasa kwani kibiashara haitaweza kuwanufaisha.

"Kibiashara hatukuwahi kumfikiria Nikki Mbishi lakini One Incredible alikuwepo kwenye orjino ya 'SSK' lakini pia waliungana na kina Stereo kutengeneza kundi lao linaloitwa 'Sisi' kwa hiyo kibiashara haipo sawa huwezi kuwa na makundi mawili yote yanaanza na sisi, tutaangalia kwanza kama haitoathiri biashara basi watakuja kujiunga hapo baadae inategemea na sapoti ambayo tutakuwa tunaipata." -Wakazi

SSK ni kundi ambalo  linaundwa na Wakazi, P The Mc , Cjamoker pamoja na Zaiid ambao wameamua kufanya kazi kwa pamoja ili kuweza kurudisha asilimia 50 ya mapato wanayopata kupitia muziki wao  katika jamii inayowazunguka.

Mtazame hapa chini Wakazi akitoa sababu.