Saturday , 4th Mar , 2017

eNewz ya EATV imewafuma LIVE wasanii wa bongo fleva Madee na Lulu Diva wakiwa wawili tu ndani ya gari, ambapo Madee amesema kuwa wamekutana kwa ajili ya shughuli za kimuziki na si vinginevyo.

Madee na Lulu

"Sisi tumekuja kwa mambo yetu ya muziki hivyo watu wasije wakaweka unafiki kwenye kuwavurungia mahusiano kwa kuwa Lulu ana mchumba wake na mimi nina girl frend wangu ambaye anampenda sana Lulu Diva, pia". Amesema madee

Kwa upande msanii wa bongo fleva Lulu Diva amepangua skendo zinazoendelea kuhusu yeye na Madee kuwa kwenye mahisiano, na kusema kuwa yeye msanii huyo ni marafiki wa karibu tangu siku nyingi na huwa akikwama mambo mengi huwa anamtafuta ili amsaidiane.

Hata hivyo Lulu alimalizia kwa kusema hana wasiwasi na Madee kwa kuwa ni  kaka yake kwenye muziki tangu siku nyingi na pale anapopata tatizo lolote huwa anamfuata Madee kwa ushauri. 

Itazame hapa