Monday , 30th May , 2016

Baada ya wasanii wa Bongo Fleva Shilole na Vanessa kujaribu kutengeneza kiki kwa ajili ya kutengeneza antensheni za mashabiki zao ambao walikuwa wakizani ni ugomvi wa kweli jana wameamua kumaliza mchezo wao.

Msanii wa Bongo Fleva Vanessa Mdee

Wasanii hao ambao walikuwa wakionekana wakijibizana katika mitandao ya kijamii pasipo na kufahamika chanzo cha ugomvi wao juzi waliamua kulishana ugali jukwaani kwa mahaba yote ili kuwadhihirishia mashabiki wao kuwa zote zile zilikuwa ni promo tu za shoo yao.

Pia Msanii Kr Mulla aliamua kufunguka wazi kuwa kama asingelikuwa msanii yeye sasa angekuwa ni mtu wa kuiba mifukoni mwa watu tofauti tofauti ambao wangelikuwa wanamkalia sawa katika taimingi zake.