Friday , 9th Oct , 2015

Mwanadada anayefanya vizuri katika muziki wa Bongo Fleva ambaye pia ni moja ya majaji wa mashindano makubwa ya kucheza Afrika Mashariki ya Dance 100% Queen Darleen,

amesema ushindani uliopo kwenye soko la muziki hivi sasa, ni moja ya kitu kinacho msababisha yeye kuchelewa kutoa nyimbo mpya kwa kuhofia kutofanya vizuri.

Queen Darleen ameyasema hayo kwenye Planet Bongo ya East Africa Radio, na kuleza kwamba kama msanii lazima uangalie jinsi hali ya soko la muziki lilivyo kwanza, na sio kukurupuka unapoachia kazi mpya.

"Unapotoa wimbo kuna ushindani, mwengine atataka kufanya kama wewe unavyofanya, kwa hiyo unampa nafasi yeye je atavuka!? mwisho wa siku havuki alafu mi naachi kitu kingine kikali zaidi ya vile alivyovitoa yeye. Mtu anaweza akatoa kazi nne tano na zote zikafeli, lakini mi nikitoa kitu nafanya kwa uhakika na ndio maana natoa audio na video kwa pamoja", alisema Queen Darleen.

Pia Queen Darleen amesema kitendo cha wasanii kutoa wimbo alafu kuja kutoa video yake baadae, ni moja ya kitu kinachowachosha mashabiki na hivyo wajipange kabla hajaachia kazi yoyote.

"Video miezi mitatu miezi minne unakuwa unawachosha mashabiki zako, atleast ukae ujijue kwamba mimi natulia lakini muda wangu ukifika wa kuachia kazi naachia kazi kweli", alisema Darleen.