Friday , 7th Mar , 2014

Ushahidi zaidi umeendelea kutolewa katika kesi ya Oscar Pistorius ambapo jirani wa karibu wa mwanariadha huyu, Dk. Johan Stipp ametoa ushahidi wake kuwa siku ya tukio alikuwa wa kwanza kufika eneo la tukio baada

Ushahidi wa Dk. Stipp unakuja kama ushahidi wa muhimu unaoweza kumuokoa Oscar ukifuatia ule awali wa jirani aliyesisitiza kusikia mayowe ya mwanamke kabla ya kusikia milio ya risasi, kitendo kinachoashiria kuwa Oscar alipishana maelewano na mpenzi wake na kupelekea kuamua kumpiga risasi.

Kesi hii bado inaendelea ambapo mwanariadha Oscar na timu ya wanasheria wake wanajaribu kwa nguvu zote kujinasua katika shtaka la mauaji ya mwanamitindo na muigizaji aliyekuwa mpenzi wake Reeva Steenkamp kwa kumshambulia na risasi, tukio lililotokea mwaka jana.