Friday , 20th Nov , 2015

Katika kuelekea siku kubwa kabisa ya maonesho ya mitindo ya Mavazi ya Swahili Fashion Week kwa mwaka huu, usahili wa wanamitindo watakaoshiriki kuonesha mavazi ya wabunifu umepangwa kufanyika siku ya kesho kuanzia saa 8 kamili za mchana jijini Dar.

Maonyesho ya mitindo ya Mavazi ya Swahili Fashion Week

Usaili huo ambao utakuwa ni mkubwa umepangwa kufanyika katika hoteli ya Colloseum iliyopo Masaki jijini Dar es Salaam.

Hii inakuwa ni nafasi ya pekee kwa wale wote wenye ndoto za kufika mbali kupitia uanamitindo, Swahili Fashion Week ikiwa na rekodi ya kuibua vipaji vya wabunifu mahiri wanaofanya vizuri kwa sasa akiwepo Nadya, Ben, Jihan na wengine wengi.
Kama wewe ni mwanamitindo na unajiamini kuwa unaweza tukutane kesho pale Colloseum.

Swahili Fashion Week kwa mwaka huu itafanyika kuanzia tarehe 4 mpaka 6 Desemba ikiwa inaletwa kwako kwa udhamini mkubwa kabisa wa East Africa Television (EATV) pamoja na East Africa Radio.