Siku ya Ukimwi Duniani (world Aids Day)
Katika siku hii kubwa duniani mastaa mbalimbali wametoa angalizo na pia nasaha kwa jamii kwa ujumla kuendelea kuwa makini kupambana na maambukizi mapya ya ugonjwa huo.
Tunda Man, vilevile Pam Daffa wamekuwa ni sehemu ya wasanii ambao wamezungumza kuhusiana na suala hilo, wakigusia pia watu, hususan vijana, wajawazito na wale waliopo katika mahusiano kufahamu kuwa gonjwa hilo bado lipo na kuzidisha umakini kujilinda.