Thursday , 27th Feb , 2014

Mwigizaji maarufu wa nchini Nigeria, Uche Ogbodo baada ya tetesi kusambaa kwa siku kadhaa juu ya yeye kuwa na ujauzito, ameamua kuibuka na kuwathibitishia mashabiki wake kuwa ni kweli anatarajia mtoto na yeye pamoja na mume wake wana furaha sana juu ya suala hili.

Tangu kuanza kwa uvumi wa tetesi za ujauzito wa msanii huyu, imekuwa ni adimu sana kwake kuonekana katika mishe zake za kila siku, na hii ni kutokana na jitihada za siku nyingi za msanii huyu kufanya mambo yake chini chini mbali na vyombo vya habari.

Msanii huyu alifunga ndoa na mchezaji mpira maarufu wa kipindi cha nyuma wa huko Marekani, Apo Arthur, na ujio wa mtoto katika ndoa hii ni ishara nyingine ya kuendelea kuimarika kwa mahusiano yao.