
msanii wa nchini Marekani Talib Kweli
Rapa huyu kupitia ukurasa wake wa Twitter amewatangazia mashabiki wake Afrika Mashariki juu ya ujio wake huu mkubwa, katika ziara ambayo ataianzia Afrika Kusini tarehe 3 mwezi Octoba.
Ujio wa supastaa huyu nchini Kenya, unatangulia ule wa rapa 2 Chainz ambaye naye atatua kuzikonga nyoyo za wapenda burudani mwezi wa 11 mwaka huu.
