Thursday , 17th Nov , 2016

Muandaaji na mtayarishaji wa nyimbo za bongo fleva Monagenstar amesema studio ya CLASSIC SOUND haija fungwa japo kwa sasa kuna marekebisho yanayofanyika katika studio yake kwa ajili ya kazi mpya.

Monagenstar

 

Akipiga stoty ndani ya eNewz Mona amesema yupo kwenye hatua ya kuandaa wasanii na ma'producer kwa ajili ya mwakani kwa kuwa mwaka huu alikuwa kimya kwa muda mrefu na sababu ikiwa ni kuandaa kazi mbalimbali kwa mwaka 2017.

Hata hivyo Mona amesema studio ya CLASSIC SOUND ilianzishwa rasmi kwa ajili ya wasanii chipukizi na wazo lake hilo lilikuwa tangu anaanzisha studio hiyo hakuwa na lengo la kufanya kazi na wasanii ambao tayari wamefanikiwa.