Tuesday , 19th Aug , 2014

Mtayarishaji muziki maarufu kutoka nchini Uganda, Steve Jean ameibuka na madai kuwa, wimbo maarufu wa msanii Bebe Cool, Love You Every Day ulichukuliwa studio kwake bila idhini yake.

Mtayarishaji muziki wa nchini Uganda Steve Jean

Steve ambaye ndiye mmiliki wa studio maarufu ya Fenon huko Uganda, amesema kuwa, kazi hii ilitoka kutokana na mpango ambao Bebe Cool aliusuka na mtayarishaji mwenzake, Michael Fingers bila yeye kuwa anafahamu.

Hata hivyo Steve amesema kuwa, hana mpango wowote wa kuchukua hatua dhidi ya hili, na kama ilivyo kwa watu wengine, yeye binafsi anafurahia mafanikio makubwa ambayo rekodi hii inaendelea kuyapata.