
Mtangazaji wa kipindi cha Planet Bongo Dullah akiwa na mwanamuziki Stara Thomas katika studio za East Africa Radio.
Stara Thomas alisema haya kupitia kipindi cha Planet Bongo na kudai wasanii wengi wanashindwa kurudi kwenye biashara ya muziki kutokana na kukata kwa mitaji ya kuweza kufanya biashara hiyo kutokana na vitendo vyao kama ulevi pamoja na kuendekeza mapenzi.
"Kuna vitu vingi vinavyopelekea mtu kushuka kimuziki kwanza ni 'mind set' ya mtu mwenyewe lakini unajua mwanamke kama mwanamke ikifika mahali akiendekeza sana mapenzi lazima ashuke, vilevi wanakula wengine unga, wanakunywa pombe sanaa kwa hiyo wanashindwa kuangalia biashara yao hiyo maana muziki sasa ni biashara, mara anakuja kushtukia msingi wake wa biashara hiyo umekata" alisema Stara Thomas.